- 20 - 25 =Iwe kama ni kielimu hujafikia malengo yako,sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya,pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.
- 25 - 30 = Hakikisha uwe na angalau na SHUGHULI RASMI kama umeajiliwa au umejiajili.
- 30 - 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja,tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa kama sio kuishi nae,tena si mbaya ukawa umeshatengeneza familia,kwa maana ya kuwa na watoto kama mungu kakuwezesha.
- 35 - 40 = Ni umri wa kama kiwanja kiwe kimejengwa, na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia.
- 40 - 45 = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja au kujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki,kama umegundua mkeo hazai fanya mchakato kwingine kama ni mwanaume na kama mwanamke umegundua mumeo ndio mwenye shida basi tafuta nje umletee mtoto. Kifupi ni umri wa masahihisho.Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa kama ni wale watoto wapo kwenye level tofauti za elimu,kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.
- 45 -50 = Kwa yule ambaye hakukosea huko nyuma,basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako,kama ni shuguli zako ni kuanza kuwahusisha,huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fulsa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 -40.
- 50 - 60 = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na shughuli za shulba.Na kama ulijitenga na msikiti/kanisa huu ndio muda wako.
- 60 - 70 = kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.
- 70 - 80 = kula matunda.
- 80 - n.k= unamsikilizia Mungu anasemaje
Home » Makala »
Mitandao Ya Kijamii
» KUTOKA WHATSAPP: Mchanganuo wa umri na kile unachotakiwa ANGALAU UWE NACHO KIBONGOBONGO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)