Kadri nyumba inavyozidi kujengwa kwenda Juu, ndo kadri kazi ya kupandisha vitu juu ya Nyumba inaongezeka, na ndo kadri ya setting mbali mbali zitahitajika kupata balance, msaada na uwezo wa kujenga kwa Juu. Siku zote kitu kizuri kinatokana na msingi imara, hata nyumba ya ghorofa ikiwa na.msingi mbovu ipo siku itaanguka tu, kwakua mmiliki aliyejenga nyumba kwa ubahili wa vifaa bora na fundi aliyejenga kwa Vifaa vibovu ili amuibie boss wakw wote ni wabomoaji wa Baadae ambao sasa wanajihisi wanajenga.
Ukubwa wa Mafanikio ya Mtu ni sawa na ukubwa wa Kujitoa kwake Kufikia mafanikio hayo. Jinsi unavyojitoa, unavyopambana kufikia mafanikio yako, ndivyo jinsi utakavyoyafikia kutokana na kujitoa kwako. Hakuna kitu kinachokuja kirahisi, labda uwe umepewa, na kama ukipewa hutajua thamani ya kuhangaikiwa kwake na hivyo utakipoteza au utakupunguza thamani kwakua labda haujui bei yake au utunzaji wake au upatikanaji wake.
Ukitaka kuwa Bilionea jitoe kupambana ya level ya Mabilionea. Ukitaka njia ya Mkato ili uhisi umewafikia wenye mafanikio, Jitoe kukopa bila Malengo. Ukutaka Kuamini kufeli kupo, basi Fungua mradi au Biashara kwa kukurupuka. Na Ukitaka Kuamini Malipo ni hapa hapa duniani, basi jaribu kwa makusudi kukatisha ndoto au mafanikio ya Mtu. Kila aliyefika Juu Hakika ameanzia chini, japokua tunatofautiana ni chini kiasi gani.
By Man Dea