Dar es Salaam. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan leo (Alhamisi), ameongoza mamia ya waombolezaji waliofika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA), kupokea mwili wa Spika wa Bunge mstaafu, Samwel Sitta.
Samia amewaongoza waombolezaji hao na kuupokea marehemu uliowasili katika uwanja huo saa 9.00 alasiri kwa ndege ya Shirika la Emirates, kutoka Ujerumani.
Sitta alifariki dunia mapema wiki hii akiwa nchini humo alikokuwa akipatiwa matibabu ya saratani ya tezi dume.
#mwananchi