MUDA WA VIJISABABU UMEKWISHA ZIFANYIE KAZI NDOTO ZAKO

Naimani nikikuuliza leo hii je tangu uanze kutupa vijisababu vya kwa nini unashindwa zifanyia kazi ndoto zako au mawazo, je vijisababu hivyo vishawai kukusogeza hata hatua moja mbele kimafanikio natumai jibu litakuwa HAPANA.



Hapana kwa kuwa vijisababu vyako visivyo na kichwa wala mkia kamwe haviwezi kukuletea mafanikio unayoyataka. Na ndio maana mpaka leo tumemaliza siku 183 kati ya 365 lakini bado uko pale pale husongi mbele. Embu leo amka kitofauti, embu leo amka na NJAA YA KUTAKA KUFANIKIWA licha ya kuwa mafanikio hayaji papo kwa hapo.

Lakini leo amka ukiwa mpya, kataa pepo linalokusukuma kuwa na vijisababu visivyo na msingi. Kumbuka unaposema una maisha magumu kuna mamilioni ya watu wana maisha magumu zaidi yako lakini bado wana PUSH FORWARD, bado wanazifanyia kazi ndoto zao.....

SO WHAT'S YOUR EXCUSE? Kuna watu hawakuwa na MTAJI lakini walijua wapi pakupeleka Mawazo yao na wakaata Sapoti iliyowawezesha ku-MOVE FORWARD, tatizo lako hutumii Fursa zinazojitokeza, huishughulishi AKILI YAKO kujua utoke vipi kwenye hali uliyonayo. Umebaki kusema nitafanya Kssho As If Una uhakika kesho utafika (hakuna Guarantee kuwa kesho tunaweza kufika, ANZA LEO).

Kuhairisha kwako mambo, vijisababu vyako visivyo na kichwa wala miguu kamwe havitoweza kukutoa hapo ulipo. It's either You stay there forever blaming and blaming ukiendelea kuwa masikini daima or YOU CHANGE THE SITUATION. Maamuzi ni yako. Kuendelea kuukumbatia Umasikini au kuamua kutoka hapo ulipo.

Instagram: @erinoebusinessconsultancy