Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema, Diwani wake Ally Bananga na Dereva Junior Mtatiro wanusurika kutekwa na wanaohisiwa kuwa majambazi baada kidogo ya Makuyuni waliopanga mawe barabarani usiku wa kuamkia leo.
Lema na watu wake walikuwa wakitokea Dodoma kuelekea Arusha ambapo mke wake anasakwa na Polisi kwa kinachodaiwa kuwa amri ya RC, na kukuta majambazi hao wakiwa wameteka Fuso na wamelizibia barabara, ndipo dereva wa Lema akafanikiwa kugeuza gari na kurudi Makuyuni mjini japo walishambuliwa kwa mawe bila kuleta madhara.
![]() |
Lema akiwa Kituo cha Polisi |
Pichani, wapo kituo cha Polisi Makuyuni kuomba msaada wa askari ambao walitangulia mbele kuwaescot .