MKUU WA MKOA AWASHIRIKISHA VIONGOZI WA DINI KUKAGUA UJENZI UWANJA WA NDEGE WA SONGWE

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo amefunga na  viongozi wa dini kukagua ujenzi wa uwanja wa Ndege wa kimataifa wa  Songwe na kupata maelezo ya uendeshaji wa shughuli katika uwanja huo.



Amesema ameamua kuwashirikisha viongozi wa dini ili wajue jitihada za serikali na wao waeleze mafanikio na Mipango ya serikali ktk kuwaletea wananchi maendeleo.

Amesema kukamilika kwa uwanja huo kutafungua fursa nyingi za kiuchumi kwa watanzania kwani nchi Nyingi za kusini mwa Afrika watatumia uwanja huo.

Uwanja huo ni mkubwa na una uwezo wa Ndege kubwa kama Airbus kutua na Ndege za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 500 hivyo itasaidia kusafirisha Maua , matunda   Na mbogamboga nje ya  nchi moja kwa moja kutokea uwanja wa Ndege Songwe.