Msanii TID awashutumu Clouds kumdhulumu katika kazi zake za Muziki

Msanii mkongwe wa muziki Khalid Mohamed aka TID ameingia kwenye mgogoro na kituo cha redio cha Clouds FM baada ya kukituhumu kituo hicho kimejiingizia fedha kwa kuhadaa wao ndio waliotayarisha wimbo wa Zeze.

Khalid Mohamed aka TID 


Leo katika akaunti yake ya Instagran alipost picha ambayo inaonyesha kuwa kazi za TID zilikuwa zinasimamiwa na Clouds na kufanyika katika Studi  za Clouds kitu ambacho TID hakijampendeza. TID amepost kava ya CD hiyo.



Alichoandika TID mtandaoni HII NI DHULUMA YA WAZI WAZI HUU WIMBO UMEFANYIKA KWELI CLOUDS MALIPO YOTE YAMELIPWA CLOUDS....BRAZA RUGE NAOMBA HELA ZANGU hivi Clouds FM mshawahi Kutenengeneza Zeze Song. .!? I WANT MY MONEY SHOW ME CONTRACT naomba Hakuna Yangu Sikuogopi I want Clouds FM kwa  Kudanganya hivi wanilipe Milioni  Mia Tano ....Ushapata Pesa Nyingi Sana Hauna Haja ya kuendelea,My Legal Team is Ready to Bring this Fake Institution Down