NIKKI WA PILI : Mashabiki Wabishane kuhusu Muziki na sio nani Namba Moja

Leo katika Kipindi cha Ladha 3600 cha E-Fm mtangazaji Jabirsaleh alikuwa na Mahojiano na Mwamuziki wa Hip hop kutoka Kundi la Weusi. Moja ya vitu ambavyo walizungumzia ni kuhusu mapambano katika Muziki wa Bongo Fleva. Na Nikki wa Pili alikuwa na haya ya kusema.

Nikki wa Pili


Nikki wa Pili alisema “Unapoona mtu amesema Fulani namba moja huna haja ya 'Kudebate' hii inatokana na maoni vile ambavyo mtu anaona na anapima kwa vigezo vyake, Msanii wa HipHop anapokuwa na Top Track sote tunapaswa kufurahia”

Pia akaongezea kuhusu "Mimi sikatai mashabiki kubishana ila wabishane kuhusu muziki sio nani kakaa wapi anafanya nini, ningefurahi kama wangebishana kuhusu show, ubunifu"