RC, DC WA MKOA WA SHINYANGA NA KAHAMA WATUHUMIWA

Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige amesema viongozi mkoani Shinyanga na wilayani Kahama wanatakiwa kuchunguzwa kwa madai ya kutumia vibaya misaada ya waathirika wa mafuriko mwaka jana.



Alidai bungeni jana kuwa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ali Rufunga na  Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya walitumia madaraka yao kujinufaisha kwa fedha za waathirika hao wa eneo la Mwakata.

Katika swali la nyongeza, Maige  alitaka kujua utaratibu utakaotumika kuwachunguza viongozi hao na ikiwezekana warudishe michango waliyochukua na kuitumia bila ya kuwafikishia walengwa. “Eneo la Mwakata Mei 3, 2015, kulitokea mafuriko na watu 47 walipoteza maisha, lakini viongozi niliowataja walitumia vibaya misaada ile, kwa nini wasishughulikiwe waliko?” alihoji.

#Mwananchi