Albert Msando ameandika haya kwenye kurasa yake ya Instagram
Mungu ni mwema. Nimempata kijana Edson Mwakyombe ambaye jana alilia kwa huzuni na uchungu kukosa mkopo ili aendele na Elimu ya Juu. Nimekutana nae Chuo Kikuu Mlimani. Ni baada ya kuweka post kuhusu Elimu ya Juu kijana huyu ambaye mama yake anaishi Mfinga Iringa na hana ndugu Dar Es Salaam leo amepata mama @isariaclothingboutique na kaka @furnituremart_ ambao wamejitolea kumlipia ada mwaka wa kwanza na wa pili. Nawashukuru sana kwa moyo wao wa kujitolea. Tuendelee kuwasaidia na wengine ambao wanalia na kuhuzunika bila msaada. Ni wengi lakini kila anaeguswa ajitoe na kumsaidia yule mwenye kuhitaji. #LetUsHelpEdoLearn #IsariaMlaki #AndrewKomba - by @albertomsando
![]() |
Kijana mwenyewe huyo aliyevaa Begi akiwa na Wasamaria wema |