SHIRIKA LA POSTA LAIDAI SERIKALI MABILIONI

Dar es Salaam. Shirika la Posta nchini limesema linaidai Serikali na taasisi mbali mbali jumla ya Sh9.2 ikiwa ni malipo ya huduma mbali mbali linazozitoa kwao.



Akizungumza na waandishi wa habari leo (Alhamisi), Kaimu Posta Masta Mkuu wa shirika hilo, Fortunatus Kapinga amesema, deni hilo linachangia posta kukosa ufanisi.

Ameainisha mchanganuo wa madai hayo kuwa, Shbil 5.5 ni deni la Serikali kwa huduma wanazozitoa kwa taasisi zake, Shbil 1.8 kwa huduma wanazozitoa kwa nitabaki ya Serikali na Shbil.1.9 ni deni kwa taasisi zisizo za kiserikali.

Naye mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk Haruni Kondo amesema shirika la posta kwa kushirikiana na menejimenti itakutana na kupitia mkataba yote ili kuibaini ile isiyo na tija na kuchukua hatua stahili.