Tamasha Kubwa la Instagram Party wanakuletea Tuzo (INSTA AWARDS), Tuzo za Kwanza Duniani kwa Watumiaji wa Instagram

Kupitia kwa Mkurugenzi wa Frecon Ideaz ambao ni waandaji wa Instagram Party wamekuja kitofauti Msimu baada ya Kuzindua Rasmi Tuzo za Instagram. Tamasha hilo ambalo litafanyika Mwezi wa 11 tarehe 26



Kwenye akaunti ya Instagram wameandika haya 

Tunataka kuongeza thamani kwako na event uipendayo @instagrampartytz kwa kutambua uaminifu wako na kuwa mtumiaji bora wa mtandao wa Instagram  hadi leo. Tupo katika harakati za kutambua wale wanaoleta mchango chanya katika mitandao ya kijamii kwa kukupa nafasi wewe mtumiaji kupendekeza na kuwapigia kura wale ambao wewe na jamii kwa ujumla inawafikiria wanastahili Tuzo hizi. Asilimia 100 washindi watapatikana kwa uwazi na kwa njia zitakazomridhisha kila mshiriki na mpendekezaji. Hivyo basi tuwape taarifa wengine wote huku tukiendelea kupata taarifa na vipengele vya Tuzo hizi kwa mara ya kwanza kufanyika Duniani.

We are about to add value to both you and your favorite event @instagrampartytz by recognizing your loyalty of being an awesome instagram user since then. We are about to Spotify those who bring impact on our social life by giving you an opportunity to bring them live (nominating) and then vote for who you and the majority think they deserve it. Make all your friends aware as we wait for further information concerning these awards taking place for the first time in the World.  #TzAllstars16 #TzInstaAwards #Ideaz16