Walichoongea Kocha Mpya Yangan Lwandamina na Hans van Plujin

Baada ya Tetesi za Muda mrefu kuhusu kocha Mpya wa Yanga Mzambia Lwandamina kutua Yanga. Hatimaye Siku ya Jana amekabidhiwa Mikoba hiyo na Mkataba wa Miaka Miwili toka kwa Hans van Plujin aliyekuwa Kocha wa Yanga. Hans van Plujin atabaki kuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Lwandamina atakuwa Kocha Mkuu wa Yanga.



Baada ya Makabdhiano ya Timu Kocha wa zamani wa Yanga Hans van Plujin aliongea na Lwandamina naye akaongea  baada ya kukabidhiwa Timu.

Mkurugenzi mpya wa ufundi wa klabu hiyo Hans van Plujin alisema
" Sinashida na majukumu yangu mapya  kikubwa nipo Yanga na nitaendelea kutimiza majukumu yangu kwa mujibu wa mkataba wangu na nitapambana na kushirikiana vyema na Mwalimu George pamoja na wachezaji na benchi zima la ufundi kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu na kufika mbali kimataifa" 

 Kocha Lwandamina alisema haya baada ya kutambulishwa:
"ni changamoto mpya kwangu najua Yanga ni klabu kubwa nitahakikisha natumia kila kinachowezekana kuhakikisha tunafanya vizuri kuanzia kwenye ligi ya nyumbani hadi klabu Bingwa Afrika.