BENKI AFDB YAIPATIA TANZANIA MKOPO WA BILIONI 360

Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) imeipatia Tanzania mkopo wa Shilingi Bilioni 360 kwa ajili ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2016/17 pamoja na kuongeza mtaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini-TADB.



Uhai wa mikopo yote miwili utakuwa ni miaka 40 ambapo Serikali itaanza kuilipa baada ya miaka kumi tangu kutolewa kwake, huku riba yake ikiwa chini ya asilimia 1.