![]() |
Jay Dee na Ruge |
Sasa habari kubwa kwa sasa ni kauli ya Management ya Lady Jaydee ikiwa ni baada ya Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Ruge Mutahaba kusema kwamba nyimbo za Jide zinaweza kuendelea kupigwa iwapo yeye mwenyewe ataruhusu maana alikataza na jina lake lisitajwe.
Uongozi wa Jay Dee umetoa taarifa na Kusema kuwa ni Ruksa kwa Clouds Media Group kuanza kupiga Nyimbo za Jay Dee muda wowote. Na kwamba wagange yajayo na kusahau yaliyopita.