LOWASSA: VIKAO VYA NDANI NI VITAMU KULIKO VYA NJE

Mafunzo hayo yanaendeshwa na chama hicho kwa kushirikiana na Taasisi ya Konard Adenauer Shiftung (Kas) ya Ujerumani.

Lowasa


Rais John Magufuli alipiga marufuku mikutano na maandamano ya kisiasa, akisema wapinzani wajiandae kwa ushindani wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020 na Jeshi la Polisi likatekeleza amri hiyo, likizuia kwa kusema inahatarisha amani, inalenga kushawishi wananchi kutotii maagizo ya Serikali na wakati fulani polisi ilitumia ugonjwa ulioua watu sita mkoani Dodoma kuzuia hafla ya Chadema.

Vyama vya upinzani vimepinga kwa nguvu amri hiyo, vikisema inakiuka katiba ya nchi, Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni za Vyama vya Siasa. Hata hivyo, Serikali imelegeza zuio hilo kwa kuruhusu mikutano ya ndani na ya wabunge kwenye maeneo yao.
#Mwananchi