MAKAMBA: ZAIDI YA HEKARI 250,000 ZA MISITU ZINATEKETEA KILA SIKU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba amesema zaidi ya hekari 250,000 za misitu huteketea kila siku nchini.

January Makamba


Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari ofisini kwake leo Waziri Makamba amesema uharibifu huo ni wa kiwango cha juu na usipodhibitiwa utasababisha sehemu kubwa ya nchi kuwa jangwa jambo alilosema ni hatari kwa Taifa.

"Katika Afrika ya Mashariki Tanzania ndiyo inayoongoza kwa uharibifu wa mazingira...hii inaiweka nchi katika hatari ya kuwa jangwa," alisema

Makamba amewataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kutoa kipaumbele kwa habari na kuzipata u muhimu habari zinazolenda kulinda mazingira nchini.