MAMBO AMBAYO ANASHUKURU SHAMSA FORD NDANI YA MWAKA 2016 IKIWEMO KUPATA MUME

Shamsa Ford ambaye amefunga Ndoa na Mpenzi wake Rashid maarufu kwa jina la ChiddMapenzi ameandika ujumbe huu kushukuru kwa Mungu kwa mambo ambayo amemtendea katika mwaka 2016.


Alichoandika Shamsa Ford
Asante Mungu kwa huu mwaka 2016.umenitendea mengi ambayo siwezi kusema chochote zaidi ya kusema asante Mungu. nilikuwa na ndoto nyingi sana ndani ya 2016 lakini hukuweza kunitimizia vyote labda kwasababu muda wake haujafika. lakini nakuomba nikushukuru kwa haya uliyonitimizia (1 asante Mola wangu kwa afya njema uliyonipa na pumzi za kupumua kila siku(2 asante Mola wangu kwa riziki unazonipa zinasaidia kuendesha familia yangu (3 asante Mola wangu kwa familia yangu ipo salama (4Asante Mola wangu kwa mume bora uliyenipa. Anaweza akawa ni mtu wa kawaida tu kwa wengine na pia wakamdharau lakini kwangu ni zaidi ya mume .hakika ni mume ambae nampenda na sichoki kumpenda. Mwenyezi Mungu naomba kifo tu ndo kinitenganishe na Rashidi wangu. Ni wewe pekee Mwenyezi Mungu ndo unayejua tunavyopendana na mume Wangu. Akinikosea naomba unipe moyo wa kumsamehe na mm nikimkosea naomba umpe moyo wa kunisamehe. (5 asante Mwenyezi Mungu kwa kila kilichonitokea 2016 .kila kilichonitokea kina sababu ndani yake .(6 Asante Mwenyezi Mungu kwa kunipa moyo wa uvumilivu kwa yote yaliyonitokea ndani ya 2016.nimejifunza vitu vingi sana katika maisha yangu haswa kutomuamini mtu yeyote katika maisha yangu. .(7 Asante Mwenyezi Mungu kwa mashabiki wa ukweli ulionipa naomba uzidi kuwabariki ...Inshaallah Mwenyezi Mungu naomba utupe afya njema ili tuuone 2017..i love you all