MAXENCE MELO AWAHAKIKISHIA USALAMA WA TAARIFA KWA WATUMIAJI WOTE WA MTANDAO WA JAMII FORUM

Baada ya kuchiwa leo kwa dhamana Mwanzilishi mwenza wa JamiiForums, Maxence Melo amesema mtandao wa JamiiForums haujatetereka na bado uko ngangari na amewataka watumiaji wote wa mtandao huo waondoe hofu kwa kuwa taarifa zao za siri ziko salama.

Maxence Melo


Pia amesema hana ugomvi wowote na vyombo vya dola na ana imani na mahakama za hapa nchini kuwa zitamtendea haki katika kesi yake.

Amewataka wananchi wote bila kujali itikadi zao kuendelea kupigania uhuru wa kusema na kutoa maoni, pia amevishukuru vyomo vyote vya habari na wanahabari kwa kumuunga mkono kipindi chote alipokuwa mahabusu.

#source #JamiiForum