MWENDO KASI WAPONZA MADEREVA 277

Dar es Salaam. Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani ,Mohamed Mpinga amesema madereva wa mabasi zaidi ya 277 wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuendesha magari kwa mwendo wa zaidi ya kilomita 90 kwa saa.



Madereva hao walikamatwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Geita, Arusha, Kilimanjaro, Kagera, Mara, Tabora, Lindi, Iringa, Shinyanga, Rukwa na Njombe baada ya operesheni iliyofanyika wiki tatu na ambayo inaendelea katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Mpinga amasema operesheni hiyo imefanyika katika barabara kuu zote, stendi za mabasi mikoa yote kwa kukagua ubora wa mabasi, mikanda, kuwapima madereva ulevi na uzidishaji wa abiria na nauli.