Nyayo zilizoachwa na binadamu wa kale mamilioni ya miaka iliyopita zimegunduliwa nchini Tanzania

Nyayo zilizoachwa na binadamu wa kale mamilioni ya miaka iliyopita zimegunduliwa nchini Tanzania karibu na pahala ambapo nyayo sawa na hizo ziligunduliwa miaka ya 1970.



Alama hizo za miguu ziliachwa na binadamu wa kale walipotembea kwenye matope na majivu ya volkano yaliyokuwa hayajakauka.

Wataalamu wanakadiria kwamba viumbe ambao hujulikana kama Australopithecus afarensis, ndio walioacha nyayo hizo, na walikuwa na kimo na unene uliotofautiana.

Wanasayansi wanasema nyayo hizo zinaashiria jinsi binadamu wa kale walivyoishi.

Australopithecus afarensis ni miongoni mwa aina ya binadamu wa kale wanaofahamika zaidi na ambao waliishi kipindi kirefu.

Visukuku vya "Lucy", mwanamke kijana aliyeishi Ethiopia zaidi ya miaka 3.2 milioni, ndiye maarufu zaidi kutoka kwa kundi hilo la binadamu.
#BBC