RAIS MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI MPYA WA NEC

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).



Taarifa iliyotolewa leo (Alhamisi) na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Jaji Kaijage ameteuliwa kuongoza NEC kwa miaka 5, kuanzia Desemba 16, 2016.

Jaji Kaijage anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ambaye muda wake wa kuwa mwenyekiti wa tume hiyo ulimalizika Desemba 19, mwaka huu.