Kajala Atoa Neno baada ya Kusambaa Video inayomuhusisha Mtoto wake

Baada ya kusambaa Video ambayo inaonyesha Mtoto wa kajala kwenye mazingira tata, na baadhi wakizusha kuwa Kajala anamtafutia mwanae wanaume. Na kajala maji yamemfika hapa na....

Alichoandika Kajala Hey everyone....jamani mimi sina shida na mtu kama akinichukia au akinisema mimi kwa kitu chochote kile...kwasababu najua binadamu kuongea mmezoea..ila katika kuongea kwenu,kuingilia na kujudge my life naomba msimuingize mtoto wangu...sijawahi kumuomba mtu anisaidie kulea hata siku moja...mimi nimeona kuna video insambaa mnasema ni mwanangu na mnajua kabisa sie paula huyo ila ilimradi tu mfurahishe roho zenu...nilinyamaza...ila sasa naona mnakoelekea ni pabaya..mnahisi yeye hana moyo? Au mnahisi haumii?.mwanangu anasoma na sitaki mumchanganye na mambo yenu ya kipuuzi...vitu vibaya mnavyo muombea mwanangu viwarudie wenyewe...leave my daughter alone jamani...give us a break..fanyani tu mambo yenu yatakayofanya mpate faida katika maisha yenu na sio mwanangu....na pia mjue kua mnamdhalilisha huyo binti na sio paula tena...na huyo binti ana wazazi na familia pia...hope tumeelewana