TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli anatarajia kufanya ziara ya siku mbili Mkoani Simiyu, kuanzia tarehe 11/01/2017 hadi tarehe 12/01/2017.

Tarehe 11/01/2017 Rais Magufuli ataweka jiwe la Msingi katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu katika Mtaa wa Nyaumata Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kufungua barabara ya Lamadi-Bariadi na baadaye kuzungumza na wananchi wa Bariadi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda, mahali lilipo jiwe la ufunguzi wa barabara hiyo.

Siku ya tarehe 12/01/2017 Mhe.Rais atatembelea kiwanda cha kutengeneza Chaki kilichopo Wilayani Maswa na baadaye ataweka jiwe la msingi katika barabara ya Mwigumbi Maswa ambapo pia atazungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa.

“Kwa niaba ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu,napenda kuwaalika wananchi wote wa mkoa wetu kujitokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.John Pombe Magufuli katika maeneo yote atakayopita. Imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu @anthonymtaka.