TANZANIA: WASICHANA ZAIDI YA 800 WALIKEKETWA

Wasichana zaidi ya 800 walikeketwa kaskazini mwa Tanzania mwezi uliopita, mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga amesema. Hilo lilifanyika ingawa polisi wamekuwa wakikabiliana na utamaduni huo. Wanawake 12 wanaotuhumiwa kuhusika katika kuwakeketa wasichana hao wamekamatwa na maafisa wa polisi, mkuu huyo wa wilaya amesema. "Operesheni ya polisi bado inaendelea. Hatutatulia hadi wote waliohusika wakamatwe na kushtakiwa," Luoga aliambia wanahabari.

Eneo la Tarime, wasichana hukeketwa wakiwa na umri wa kati ya miaka 12 na 17. Inakadiriwa kwamba nchini Tanzania, wasichana na wanawake 7.9 milioni wamekeketwa. #bbc