BODABODA ZAPIGWA MARUFUKU RUFIJI

Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Pwani umesitisha usafiri wa pikipiki maaruf kama bodaboda ifikapo majira ya  jioni katika wilaya ya Rufiji

Uamuzi huo wa Kamati ya Ulinzi umefikiwa baada ya kukidhiri kwa matukio ya uharifu kwa kutumia aina hiyo ya usafiri wilayani Rufiji

Akizungumza na kamati ya ushauri ya mkoa wa Pwani (RCC) Mkuu wa Mkoa huo Evarist Ndikilo amesema kuwa hatua hiyo imetokanaa na watuhumiwa wengi wa uahalifu wilayani humo wamekuwa wakitumia usafiri huo kutoroka mara baada ya kufanya uhalifu

Usafiri huo sasa hautoruhusiwa ifikapo saa 12 jioni