Juma Nature: Afunguka Juu ya Tuhuma kutoka kwa 'Harmorapa' kuwa amemtoza Pesa Nyingi Kwenye Kolabo yake

Msanii mkongwe wa muziki nchini, Juma Nature amevunja ukimya baada ya Harmorapa kumtuhumu kumdai pesa ya mavazi kwa ajili ya video ya wimbo wake mpya ‘Kiboko Ya Mabishoo’.

“Nikisema nimemlipisha Harmorapa pesa kwa ajili ya kolabo nitakuwa nakosea. Mimi ni mtu mzima nilikubali kufanya wimbo na msanii yule kwa sababu ni mkali na anajua muziki pia na imani atafika mbali. Hawezi kunilipa mimi, ana hela gani?,” amesema Nature.

Wiki chache zilizopita, Harmo alimlalamika msanii huyo mkongwe  akisema, “Haipo sawa kwa wasanii wakubwa kutudai sisi ‘underground’ pesa ya kufanyia collabo wakati wanajua bado hata hatuanza kufaidika na muziki wenyewe.”