MauaSama amedai hakuna kitu kinachomuingizia mkwanja mwingi kwa sasa kama muziki

#MauaSama amedai hakuna kitu kinachomuingizia mkwanja mwingi kwa sasa kama muziki mpaka kufikia hatua ya kuagiza gari mpya.. amesema kazi yake ya muziki imekuwa ikimfanya aweze kujitegemea katika mambo mengi anayotaka kuyafanya akiachana na elimu aliyoipata akiwa darasani.

#MauaSama👉 “Muziki ni mzuri na ninaupenda sana  ndiyo maana unaona kila nikiimba ninaimba kwa hisia sana. Hii ni kutokana na mimi mwenyewe kuipenda kazi yangu vilevile, muziki unalipa tena sana, mimi umeweza kuniletea mafanikio mengi moja wapo likiwa ni kuagiza gari aina ya ‘IST New Model’ ambalo nategemea hivi karibuni litaingia nchini kutoka nilipoagiza”. Alisema hato kwenye PBongo EATV