Shamsa amaliza kila kitu kuhusu yeye na Gabo

Msanii wa bongo movie Shamsa Ford amesema watanzania waache kuropoka na kuongea bila kujua kinachoendelea kuhusu yeye na msanii mwenzake Gabo.




Akiongea kupitia kipindi cha eNewz, Shamsa amesema hata mume wake anaelewa kinachoendelea na hana wasiwasi na Gabo, huku akiwashukuru watu wanaosambaza taarifa hizo kwa kumsaidia kutangaza movie


"Tuache mambo ya kukurupuka kuongea kwamba nimejiweka kwa Gabo wakati hawajui kitu gani kinaendelea baina yetu ila nashukuru kwa kuwa wametusaidia kutangaza movie yetu kwani hata mume wangu mwenyewe anacheka tu" amesema Shamsa.


Shamsa amelazimika kutoa ufafanuzi baada ya hivi karibuni kupost picha akiwa na Gabo, na kumtaja msanii huyo kuwa ndiye ambaye humkosha katika uigizaji, na kwamba akiwa anaigiza naye, huhisi kama anafanya kweli.


Hata hivyo Shamsa hakusita kuongelea suala na mume wake kutajwa katika tuhuma za madawa ya kulevya na kusema kuwa kabla ya kuolewa aliambiwa atapitia mambo mengi matatizo, shida, raha na changamoto nyingi sana katika ndoa lakini anashukuru Mungu kwa kila kitu.


"Hiki ni kipidi ambacho nimekuwa karibu na mume wangu kuliko siku zote tunavyokuwa karibu" Alimalizia Shamsa.