Alichokiandika Zitto Kabwe baada ya Katibu wa Bunge kutoa Ufafanuzi

Baada ya Katibu wa Bunge kutoa ufafanuzi kuhusu uwakilishi wa vyama katika uchaguzi wa Bunge la Afrika la Mashariki, Kiongozi wa Chama cha ACT Zitto Kabwe ameandika haya kwenye ukurasa wake Facebook

"Tumepigania HAKI yetu ya kugombea kuwakilisha nchi EALA Kwa kutumia njia zote sahihi Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge. Tukishinda na kupata haki hiyo tutashukuru. Tukishindwa na kukosa haki hiyo tutatii maamuzi ya Kamati ya Kanuni. Kuna watu wanatulaumu kwa kupigania haki yetu. Tukishinda watasema tumebebwa na tukishindwa watasema tumebwagwa. Ndio binadamu walivyo, haswa binadamu wabinafsi, waliojaa chuki, husda na woga ( inferiority complex). Watu wa aina hii wanastahili jambo moja tu, KUWAPUUZA. Sisi tumetumia njia za kikanuni kutafuta tunachoamini ni haki yetu, haki ya kugombea. Tutatii maamuzi ya vikao na kusonga mbele. Hii ni ' battle ' moja tu kati ya battles nyingi Sana zilizopo mbele yetu. Katika kila battle tunajifunza, tunakomazwa na tunaweka akiba Kwa battle za mbele. Wanaona kila battle ni Zero-Sum game na kwamba wanamaliza maneno yote dhidi ya wanaowaona ni adui zao Leo na kusahau adui mkubwa zaidi, tunawaona. Tunawatazama. Tunabonyea na kuwapisha. Siku watakapoona uwiano wa 0.002 unahitajika katika VITA kubwa mbele yetu, tutapigana nao lakini ni lazima tutawakumbusha kuwa HUU NI MCHANGO wetu japo mdogo. We move on. Kwa funzo lingjne kubwa Sana kwenye harakati za kujenga Demokrasia ya Uhakika nchini kwetu.