KAMATI YA MASAA 72 YAIONGEZEA KASI SIMBA

Baada ya kusubiri mda mrefu hatimaye Kamati ya Masaa 72 imekamilisha kazi yake kwa ajili ya kuitolea maamuzi rufaa ya klabu ya Simba iliyokuwa inaihusu klabu ya Kagera Sugar baada ya kumchezesha mchezaji wake Fhaki Mohamed ambaye alikuwa na kadi 3 za njano wakati Simba ilipochuana na timu hiyo.

Baada ya taarifa hii ya kamati Fahari News imeongea na Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba Eng. Geofrey Nyange 'Kaburu' kwa njia ya Simu na  kuweza kuthibitisha kushinda rufaa hiyo ambayo inakwenda kuwaongezea point 3 na kuifanya klabu ya Simba kuongoza ligi kuu ikiwa na jumla ya pointi 61

'Tumefurahi sana sisi kama viongozi na wanachama wote wa Simba, tumekuwa wasikivu, watulivu katika kipindi chote hichi cha kusubiri majibu ya rufaa hii, na tunashukuru kwa Kamati ya Masaa 72 kutenda haki kwenye hili na hivyo kuweza kupata pointi 3 ambazo kisheria tunapaswa kuzipata. Sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye mechi yetu ya mwisho kanda ya ziwa dhidi ya Toto African'.

Simba sasa inakwenda kuongoza ligi ikiwa na Jumla ya pointi 61 huku mpinzani wake wa Jadi Yanga akifuatia na Pointi 56