MAWAZIRI WA KIGENI G7 WAKUTANA ITALIA KUIJADILI SYRIA


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amewasili nchini Italia kwa ajili ya kikao na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi saba zilizoendelea zaidi kiviwanda duniani.

Mazungumzo hayo yanatajwa kulenga pila namna ya kuifanya Urusi kujiondoa Syria katika mgogoro unaoendelea ,hii ikichagizwa zaidi na shambulizi la gesi ya sumu wiki iliyopita.

Tillerson ambaye siku ya Jumanne ataelekea pia Moscow, amekuwa akiilaumu Urusi kwa kushindwa kuzuia shambulizi hilo.
Amesisitiza kuwa kuliangamiza kabisa kundi la IS inabaki kuwa ajenda kubwa ya Marekani nchini Syria.