Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema matendo ya utekaji nyara wananchi yasipotatuliwa yatakipa shida Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
Akiwahutubia wananchi wa jimbo lake la Mtama jana, Nape alitaka hatua zichukuliwe za kukomesha tabia ya utekaji nyara wananchi, huku akikumbusha tukio la kada wa CHADEMA Ben Saanane ambaye amepotea miezi mingi iliyopita katika mazingira ya kutatanisha.