Mtoto wa Kajala Awa Kivutio kwenye Onyesho

Mtoto wa  Kajala Masanja, Paula hivi karibuni aligeuka kivutio kikubwa shuleni kwao kwenye mahafali ya kidato cha sita baada kushiriki onesho la mavazi ya Kiafrika, jambo lililoamsha shangwe kwa wahudhuriaji.

Mtoto wa Kajala


Paula Anayesoma katika Shule ya Sekondari ya Barbro, iliyopo Kibamba jijini Dar, alionesha vazi hilo la Kiafrika mbele ya mama yake (Kajala) ambaye baadaye alimkataza asishiriki tena bali ajikite kwenye masomo zaidi.

“Najua mwanangu anapenda sana urembo ila mimi sipendi afanye hivyo kwa sasa, napenda ajikite zaidi kwenye masomo na leo ndiyo mwanzo na mwisho wa kushiriki mashindano haya,”