Dar es Salaam. Rais John Magufuli amewaapisha wajumbe wa kamati maalum ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena.
Hafla ya kiapo kwa wajumbe wa kamati hiyo imefanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kamishna wa Maadili Jaji Harold Nsekela na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Kamati hiyo ya wanasayansi wanane walioteuliwa na Rais Magufuli tarehe 29 Machi, 2017 inaongozwa na Mwenyekiti wake Profesa Abdulkarim Hamis Mruma na itafanya kazi ya uchunguzi kwa siku 20 kisha kuwasilisha ripoti yake kwa Mhe. Rais