NAY WA MITEGO: HAKUNA CHA KUBADILISHA KWENYE WAPO

Emannuel Elibariki 'Nay wamitego' aliyeteka masikio ya watu wengi kupitia wimbo wake wa 'Wapo' amesema kwa sasa hakuna anachoweza kubadilisha kwenye wimbo wake huo

Nay wa Mitego mwishoni mwa wiki alikutana na  Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na michezo Dk Herrison  Mwakyembe  na kufanya naye mazungunzo mjini Dodoma

Nay alisema kwa sasa hakuna kitu anachoweza kukibadilisha  kwenye wimbo huo kwan haukua na lengo baya kwani alilenga kufikisha ujumbe  ambao tayari anaona  umeshaanza kufika sehemu husika

Alisema mapendekezo ambayo aliyatoa Rais John Magufuli, atayafanyia kazi

"Nimeitika wito wa Mh Waziri nashukuru tumeongea mengi wanasema usikatae wito kataa maneno, haikua kwa ubaya na hakuna chakurekebisha kwenye wimbo wetu wa 'wapo', ila aliyopendekeza Mh rais nitayafanyia kazi " alisema Nay Nakuongeza kuwa

"Huu ni wimbo wenu mashabiki wangu wote Tanzania na duniani kote 'wapo' ujumbe umaenza kufika,sina mlinzi wala body guarg ninyi ndio walinzi wangu "
Wimbo huo ambao awali ulidaiwa kuvuja kabla ya msanii huyo kuusambaza  katika vyombo vya habari, ulimsababishia kukamatwa na hata wimbo huo kufungiwa na Baraza la sanaa la Taifa  (BASATA ) kwa madai ya kuvunja maadili.