Nick wa Pili: Mimi ni muoga wa kupanda ndege

Umewahi kujiuliza kwanini Joh Makini na G-Nako ndio ambao hukwea pipa zaidi kwenda kufanya video Afrika Kusini huku Nick wa Pili akipenda kubaki Bongo?

Nikki wa Pili
Basi jibu limepatikana jana. Nick amekiri kuwa yeye ni muoga wa kupanda ndege na hutamani kungekuwa na namna nyingine ya kwenda aendako ili tu asizipande.
Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Nick amesema ameshapanda ndege kwa zaidi ya mara sabini lakini bado hajazizoea hata kidogo.
Nick wa Pili si staa pekee mwenye uoga wa kupaa ndege, wengine duniani ni pamoja na Miley Cyrus, Britney Spears, Ben Affleck, Dennis Bergkamp na wengine kibao.