TOTO YAIVUTA SHATI SIMBA


Klabu ya Toto African leo imeendeleza rekodi yake ya kutokufungwa na Klabu ya Simba kwa takribani miaka saba sasa pindi Toto inapocheza katika uwanja wa CCM Kirumba.

Huku ikiwa na matumaini makubwa ya kushinda klabu ya Simba leo imeshindwa kuwapa kile walichokitegemea wapenzi na mashabiki wake wengi waliojaa kwenye uwanja wa CCM Kirumba wakitazamia timu yao ya Simba kuweza kuondoka na pointi 3 katika uwanja huo.

Mpaka mpira unakwisha huku mashabiki wa klabu zote mbili wakisubiri kwa hamu timu moja wapo iweze kuona nyavu za mwenzake, Toto African 0 - 0 Simba

Sasa klabu ya Simba inaongoza ligi ikiwa na jumla ya pointi 62 huku ikifuatiwa na wapinzani wake wa Jadi Yanga wenye pointi 56.

Matokeo ya Mechi Nyingine ambazo zimechezwa leo katika viwanja mbalimbali ni

Stand United 0 - 0 Mtibwa
JKT Ruvu 2 - 2 Azam FC
Ruvu Shooting 4 - 1 Majimaji      #Ligikuuu