WADAU KUICHANGIA SERENGETI BOYS


Dar es Salaam.Kamati ya kuhamasisha Watanzania kuichangia timu ya taifa ya vijana ‘Serengeti Boys’ imeandaa hafla maalumu ya chakula cha usiku kwa ajili ya kuichangia Serengeti Boys itakayofanyika Aprili 28.

Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Soka wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFDF), Derick Mususuri aliliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam jana kuwa hafla hivyo itawakutanisha wadau mbalimbali wa michezo.
“Kampeni yetu inaendelea lakini hadi sasa sijapata takwimu za kiasi gani kilichochangwa na watanzania lakini kesho (leo) ninatumai nitakuwa nimepata taarifa kutoka kwa wenzangu juu ya ni wapi tulipofikia,”alieleza
Kamati hiyo ya watu 10 iliteuliwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye na ilipewa jukumu la kusimamia mchakato wa kuhamasishja watznania kuichangia Serengeti Boys kwa hali na mali ili ishiriki kikamilifua fainali za Afrika zitakazofanyika Gabon mwezi ujao.

Taarifa kutoka zinasema timu hiyo imeendelea na maandalizi kabla ya kucheza mechi ya kwanza ya kujipima nguvu dhidi ya Gabon wiki ijayo.