YANGA SC : Taarifa kwa Umma

Klabu ya soka ya Yanga SC inapenda kutoa taarifa juu ya safari yake hapo kesho kuelekea Algeria katika mechi ya marudiano dhidi ya Mc Alger

Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka kesho jioni majira ya saa 12 kwa ndege ya shirika la Emirate kupitia Dubai.

Wachezaji watakaondoka ni Makipa; Deogratius Munishi na Beno Kakolanya . Nafasi ya ulinzi ni ; Nadir Haroub , Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua , Juma Abdul , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani.

Nafasi ya viungo ni; Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke,Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimoni Msuva, Geofrey Mwashuiya na Emmanuel Martin.
Upande wa washambuliaji ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma

Wachezaji wafuatao wataukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali Justine Zulu,Malimi Busungu,Matheo Antony,Ally Mustapha,Pato Ngonyani ,Obrey Chirwa na Yusuph Mhilu.

Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano;
Young Africans SC
12/04/2017