Bodi ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya CCM chini ya uenyekiti wa Adam Kimbisa, imejiuzulu na kumpa barua Rais Magufuli.
Barua hiyo inaeleza kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Bodi hiyo wameamua kwa hiyari yao kujiuzulu nafasi zao.
Haya yametokea Baada ya Muheshimiwa Raisi kutembelea Ofisi za Uhuru Media na kukuta wafanyakazi hawajalipwa mishahara ya zaidi ya miezi sita ambayo inakadiriwa kufikia millioni 600 za kitanzania.