Bukombe: Mwalimu Mkuu kahukumiwa miaka mitatu na Faini ya shilingi 1.6 millioni

Mwalimu  Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja ya iliyoko wilayani Bukombe, Daniel Nying’ati (41), ambaye aliomba rushwa ya Sh130,000, atatumikia kifungo cha miaka mitatu, na akimaliza alipe faini ya Sh1.6 milioni.


Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya, Gabriel Kurwijila amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haukuacha shaka, hivyo Mahakama  inamhukumu mshtakiwa kwenda jela miaka mitatu.

















Hakimu Kurwijila amesema baada ya kumaliza kifungo, mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh1.6 milioni na kutaka adhabu hiyo iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hiyo.


Kabla ya kusomewa hukumu hiyo, akitumia nafasi aliyopewa kujitetea ili apunguziwe adhabu, mshtakiwa alisema ana familia inayomtegemea hivyo hakimu amuhurumie.
#Mwananchi