Afande Sele amlipua Zitto Kabwe kuhusu tuhuma za Ufisadi wa NSSF

Leo mwanachama wa ACT na mgombea Ubunge wa Morogoro mjini kupitia ACT Ndg Selemani Msindi (Afande Selle) ametoa maoni yake kuhusiana na chama chake cha ACT na kashfa za NSSF.
.....................................


Afande Selle anasema;

Nje ya uvyama kila Mtanzania Mzalendo anahitaji majibu ktk hili kwani kulingana na tetesi za muda mrefu kutoka kwa watu tofauti ni kwamba hata uanzishwaji wa chama chetu cha ACT ni matokeo ya matunda ya ufisadi huo mkubwa uliotendeka ndani ya NSSF ikiwa ni malengo maalum ya kuvuruga upinzani imara uliokuwepo wkt wa uchaguz mkuu na si kujenga chama/taasisi imara ya ACT..

Lengo kuu lilikuwa ni kujipendekeza kwa serekali mpya ya chama tawala kama ilivyokua ktk serikali iliyopita ya JK ambayo kupitia serikali ile uswahiba wa kiongoz wa chama chetu na mkurugenzi wa NSSF ulishamiri kupita kawaida huku upigaji wa kutisha ukitamalaki.

Lkn bahati mbaya malengo hayo hayakufanikiwa wkt wa uchaguz kwa ACT kushindwa kwa aibu ktk ngazi zote hali iliyopelekea serekali mpya kuona haina sababu ya kuibeba ACT au viongozi wake kwani haitovuna chochote na ndipo JPM pamoja na kumsifu ZZK kipindi kile aliposalia bungeni peke yake baada ya wapinzani wote kutoka nje ya bunge lkn akamtosa kwa mambo mengine tofaut JK aliyewabeba ZZK na Mr. Dau.

Hapo ndipo hasira za ZZK zikawaka na kuanza kuwa mkosoaji mkubwa wa JPM binafsi na serekali yake... Anafanya hivyo si kwa sababu ya uzalendo wake kwa nchi bali kwa sababu maslahi yake binafsi yameguswa.. 'Kweli itatuweka huru... Wacha party ianze  ...niendele ama nisiendeleeee..

Seleman Mshindi (Afande Sele)

Mwanachama wa ACT WAZALENDO na Mgombea ubunge Morogoro Mjini 2015(ACT)