Alikiba: Washindi ambao wameshinda kwenye tuzo za 'MTV Mama Awards' wanastaili




Katika ushindani kuna kushinda na kushindwa sisi hatusemi kuwa tumeshindwa na naamini Tanzania ina vipaji sana na kila msanii anajitahidi kufanya kwa uwezo wake ili aweze kufikisha nchi yetu sehemu nzuri, kwasasa muziki wetu umekuwa kwa kasi sana na unazidi kutanuka. Kwa washindi ambao wameshinda kwenye tuzo za 'MTV Mama Awards' wanastaili kwasababu kazi wamefanya na tumeziona"  Alikiba alisema

Alikiba ameyaongea haya baada kuulizwa swali na mtangazaji wa Cloudstv katika kipindi cha leo cha #Clouds360