Chanjo zilizoadimika zaanza kuwasili.

SERIKALI imetangaza kuwa chanjo ambazo zilikuwa zimeadimika nchini zimeanza kuwasili juzi na nyingine zitawasili leo.



Aidha imesema kwamba chanjo hizo zitaanza kusambazwa wiki hii.
Kauli ya kuwasili kwa chanjo hizo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Afya, Nsachris Mwamwaja.

Alisema katika taarifa yake kwamba: “Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwafahamisha wananchi kwa ujumla kwamba chanjo ambazo zilikuwa zina upungufu za pepopunda (T.T) na kifua kikuu (BCG) zimewasili Oktoba 3, 2016 na Oktoba 5, 2016 tutapokea chanjo za polio (OPV). Chanjo hizi zitaanza kusambazwa wiki hii.” Alisema kuwasili chanjo hizo, wanategemea upungufu huo wa chanjo katika baadhi ya sehemu za nchi utakwisha na wazazi na walezi wanaombwa kuwapeleka watoto wale ambao hawajapata chanjo wakakamilishe.

 #HabariLeo