D-Ommy amewataja wasanii watano ambao walipata shangwe zaidi kwenye Fiesta.



DJ wa Clouds FM na mshindi wa DJ bora Afrika kwenye tuzo za Afrimma 2016, D-Ommy amewataja wasanii watano anaodhani walipata shangwe zaidi kwenye Fiesta. “Mimi nitataja randomly tu lakini watano,” Ommy ameiambia Bongo5.

“Wa kwanza Mr Blue… Mr Blue bana ana shughuli nzito kiukweli. Wa pili Ben Pol anafanya vizuri sana, wa tatu Darassa, wan ne Fid Q, pia na Weusi,” ameongeza D-Ommy. Fiesta Dar itafanyika November 5 kwenye viwanja vya Leaders Club.

Bongo5