DARASA HURU: Umezungukwa na Watu wa aina gani ?

Hukatazwi kuwa na marafiki, hukatazwi kuzungukwa na watu mbalimbali, swali ni je hao waliokuzunguka wanakusaidia wewe kukua? Kadri unavyokua, marafiki zako wanabadilika, wengine mtapotezeana na hapohapo utapata marafiki wapya, je mnasaidiana vipi katika kukua kwenu kimaendeleo?



Marafiki ambao hawakusaidii wewe kukua ujue wanataka wakuone wewe ukibaki unatambaa milele. Marafiki ulionao wanaweza wakakusaidia kuikuza  ndoto yako au kuiua ndoto yako.

Usipende kupokea ushauri toka kwa marafiki wenye mtazamo hasi. Usipende kuwashirikisha watu matatizo yako wakati hawawezi kukupa msaada wowote hata wa mawazo.

Sio kila mtu lazima abaki kuwa rafiki yako, na si kila mtu lazima ahusike kwenye safari yako ya mafanikio kama hawastahili kuhusika.

Utajiuliza kwa nini hufanikiwi kumbe umezungukwa na watu wasiopenda ufanikiwe. Kutwa umezungukwa na marafiki wala bata wakati wenzio tumezungukwa na marafiki wenye malengo ya kutoboa maishani, wenye kuwaza kuwekeza badala ya kula bata.

Kuna msemo usemao, IF YOU RUN WITH WOLVES, YOU WILL LEARN HOW TO HOWL BUT IF YOU ASSOCIATE WITH EAGLES, YOU WILL LEARN HOW TO SOAR TO GREAT HEIGHTS.
Ukweli ambao wengi hawapendi kuusikia ni kwamba UTAKUWA KAMA WALE WATU WA KARIBU WALIOKUZUNGUKA. Na hii inahusisha hata kama umezungukwa na wanafamilia wako, mpenzi wako, ndugu yako, marafiki zako au mtu yeyote yule.

Kama waliokuzunguka wanapenda kufanikiwa, bila shaka nao watatamani wakuone na wewe ukifanikiwa na kinyume chake ni kweli.UKIFANIKIWA MARAFIKI ZAKO WATAKUJUA TU, ILA UKIFULIA NDIPO UTAKAPOJUA UMEZUNGUKWA NA MARAFIKI WAPI NA WA AINA GANI.

Usimfanye mtu Priority wakati wewe ni Option kwake na hawakusaidii kufikia malengo yako.
Ni heri kuwa na marafiki wachache lakini watakusukuma kuzifikia ndoto zako.

THE CHOICE IS YOURS ONLY. BUT REMEMBER, YOUR NETWORK BUILDS YOUR NETWORTHY.