ELIMU BIASHARA: Wajibu wa Baba ukiwa nyumbani

ELIMU BIASHARA


Dady Duty

Wajibu wa Baba ukiwa nyumbani. Sijui kwanini ukiwa mtoto unakua unapenda sana Shule yani, ila inafika Pahala we na shule mnakua si marafiki tena. Nimemiss ule uji na ndizi kisukari, na ile nyimbo ya "Saasaa saa ya kwenda kwetu, kwaheri mwalimu kwaherii, Tutaonana keshooo" Alafu unatoka nduki moja Kali sana breki ya kwanza nyumbani unahema Hoi, hawa watoto wa sikuhizi wakimaliza kuimba wanakimbili kwenye School Bus, kwanza hata hii nyimbo nahisi wanaiimba kwa Kidhungu nowdays u know.

Kuna wakati unapowaza raha ya kukaa na mwanao ndo unapokumbuka kuwa mjasiriamali, ndo unapowaza kwamba kazi ndo inakufanya utoke kwako kumi na moja mtoto kalala na kurudi saa nne usiku mtoto kalala, na Jumapili ukipata mda ni kanisani na jioni kwenye Vikao vya Harusi vya Byabato. Ila kuna mtu anaamka saa kumi na mbili, anapeleka wanae shule, alafu ndo anaenda Kufungua duka lake. Wakati anawapeleka wanae shule anawapa na semina ya ujasiriamali njiani na jinsi anavyoendesha biashara zake na kampuni zake. Mtoto kama huyu atakua akikomaa kielimu ya shule na kielimu dunia na atakua akikua akiamini katika kujiajiri na kuwekeza zaidi. 

Kila siku anapata semina kwa baba, anakia akiona Baba kamfungulia akaunt ya saving Bank, mara baba kamwekea Hela UTT, atakua anajifunza Savings pia. Watoto ni wepesi sana kuelewa zaidi wangali wadogo na ndo mana hata wahenga walisema "Samaki Mkunje angali Mbichi". Obby anampeleka mwanae stewart na pickup shule, dogo anamuuliza Baba kwanin hukununiaga hata Rav 4 kama ya kina Da zena, anaambiwa Babaako ni Mkulima na pickup inakisaidia wewe shule na mimi shamba, umesahau hata Mashudu ya Nguruwe nabebaga humu, Teach Them Young.

By Man Dea
Instagram @elimu_biashara