Jay Z kutumbuiza kwenye tamasha la Hillary Clinton

Jay Z

Rapper huyo amekubali kutumbuiza kwenye tamasha la mgombea huyo wa urais kupitia chama cha Democratic huko Cleveland. Show hiyo ambayo haijaelezewa itafanyika lini itatumika kushawishi zaidi wapiga kura wamchague.
Miaka minne iliyopita, Jay Z aliungana na Bruce Springsteen kutumbuiza kwenye tamasha la Rais Barack Obama, siku moja kabla ya uchaguzi.
Rappers kama Pusha T, Common, Chance the Rapper, na will.i.am wamemuunga mkono hadharani mgombea huyo.