Jamhuri Kihwelu "Julio" ametangaza rasmi kuacha kufundisha soka la Tanzania



Kocha mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelu "Julio" ametangaza rasmi kuacha kufundisha soka la Tanzania kutokana kuonewa na waamuzi. “Kuanzia leo na kuendelea, sitaki tena mpira. Najiuzulu mpira moja kwa moja sitaki kwa sababu mpira wa Tanzania unachezwa kwa siasa sana. Mpira unachezwa kwa ajili ya kufurahisha watu hata wasiokuwa na uwezo waonekane wanajua, hiki kitu kinaumiza sana”, amesema Julio